KAMPALA,UGANDA

UGANDA imesajili kesi mpya 65 za Covid-19, idadi kubwa zaidi iliyowahi kurikodiwa kwa siku moja ambapo idadi ya kwa sasa imefikia 1500.

Kati ya kesi zilizosajiliwa 30 ni kutoka Kampala, sita kutoka Namisindwa,saba kutoka Wakiso, 10 kutoka Tororo, Moroto, Katakwi, Buikwe, Bukwo, Bundibugyo, Mbale, Isingiro, Hoima na Buliisa.

Wengine waliobainika kuwa na maambukizi kutoka  Ethiopia, mmoja kutoka Oman na madereva wa malori 16.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA), kumekuwa na ongezeko la kesi za Covid-19 huko Kampala kufuatia kufunguliwa njia za usafiri ikiwemo barabara ambazo zinatumia usafiri wa umma na wa kibinafsi.

Waziri wa Masuala ya Kampala Betty Amongi, alisema sehemu kubwa zenye maambukizi ya  Covid-19 zilizopo Kampala ni barabara zinazotumia usafiri wa umma na wa kibinafsi, maeneo ya kazi na makaazi.

“Tumekuwa na ongezeko la asilimia 50 huko Kampala, tulifungua safu mbili za usajili zimesajili watu waliopimwa. Sehemu za kazi ni sababu kubwa ya hatari na usafiri wa umma.Idadi kubwa ya watu ambao wamepima kipimo walitumia usafiri wa teksi au  boda boda na katika eneo hili, ufuatiliaji umekuwa ngumu sana kwa sababu teksi hizo kawaida huchukua njia tatu au tano kwa siku,” Amongi alisema.