KAMPALA,UGANDA  

SERIKALI ya Uganda imeonya kuwa itarejesha tena marufuku ya usafiri wa umma kutokana na ukiukwaji wa kanuni za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, wakati idadi ya maambukizi inaongezeka kwa kasi nchini humo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Uganda Edward Katumba Wamala alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa waendeshaji wa teksi na bodaboda wanapuuza kanuni zilizowekwa na Wizara ya Afya za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, ikiwemo kuvaa barakoa, kukaa  umbali wa kijamii na kutumia vitakasa mikono.

Waziri huyo alisema Uganda huenda italazimika kusitisha usafiri wa umma kutokana na kuongezeka kwa kasi maambukizi ya virusi vya Corona,na kufanya idadi ya jumla ya maambukizi ifikie 1,500.