NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya Soka ya Uhamiaji imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la FA kwa kuwafunga Mafunzo kwa penalti 4-2.

Mchezo huo wa kiporo wa kumalizia hatua ya 16 bora ulichezwa kwenye uwanja wa Mao Zedong, ambapo kwa matokeo hayo Uhamiaji itakutana na Raskazone kwenye hatua ya robo fainali.

Miamba hiyo ilikuwa ikishambuliana kwa zamu ililazimika kupigiana mikwaju ya penalt baada ya dakika 90 kumalizika wakiwa wamefungana mabao 2-2.

Katika mchezo huo Uhamiaji ndio waliotangulia kupata mabao ya mapema na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao hayo ambayo

yote mawili walisawazishiwa ndani ya dakikia 10 za kipindi cha pili.