Ni tishio kwa akinamama wajawazito, watakiwa kuwahi kliniki mapema

NA MWANDISHI WETU

KIFAFA cha mimba (eclampsia) ni hali ya mama mja mzito kupata degedege (fits) kutokana  na kupanda kwa  msukumo wa damu (High blood pressure)  usio wa kawaida kuanzia 140/90 mmHg na kuendelea. kikawaida blood presha ya kawaida ni 120/80 mmhg.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa awamu ya saba kwa kiasi kikubwa suala la huduma za uzazi zimepewa kipaumbele ili kuona kwamba wanadhibiti vifo vitokanavyo na uzazi ikiwemo hicho cha kifafa cha mimba.

Kutokana na hali hiyo Rais Dk Ali Mohamed Shein, ameiimarisha wodi ya wazazi na watoto ili kuona kwamba wanadhibiti vifo vya mama na watoto havitokei.

SABABU ZA KIFAFA CHA MIMBA

Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 18 na umri mkubwa zaidi ya miaka 40, mama mja mzito mwenye mapacha anauwezekano mkubwa sana wakupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.

Aidha Mama mja mzito mwenye historia ya Ugonjwa wa presha, mwenye ugonjwa wa kisukari kabla ya kubeba mimba ana uwezekano wa kuugua kifafa.

Sambamba na hilo lakini mwanamke aneugua ugonjwa wa figo wakati wa ujauzito, kuaji wa kondo la nyuma (placenta).

Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba.

Pia uwezekano wa kurithi pia huchangia kupata ugonjwa huu, unene kupita kiasi kwa mama mja mzito

DALILI NA ISHARA ZA KIFAFA CHA MIMBA

Inawezekana kupata daliliza kuumwa na kichwa, macho kupoteza nuru, maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika na mkojo kuwa na rangi  isio ya kawaida.

Dalili nyengine Kupumua kwa shida,Uchovu na maumivu ya viungo, kupoteza fahamu na “degedege”, kichomi, shinikizo la damu, kuvimba na kubonyea kwa miguu (Pitting Oedema).

MATIBAU YA KIFAFA CHA MIMBA

Matibabu ya kifafa cha mimba  ni ya haraka sana ambapo ni busara juhudi kubwa zikachukuliwa ili kumwokoa mama na si vinginevyo.

Kama vile kuitowa mimba (termination) haraka iwezekanavyo bila kujali umri wa mimba hiyo.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA

Kifafa cha mimba kinaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni kama ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mama mjamzito kwa kiwango kikubwa ambacho kinaweza kumsababishia kupoteza maisha. 

KINGA ZIDI YA KIFAFA CHA MIMBA

Ieleweke kwamba mpaka sasa hivi hakuna chanjo wala tiba ya kuzuia ugonjwa wa kifafa cha mimba, ushauri mkubwa ni kuzuiya kwa wanawake  wenye umri mdogo  kutobeba mimba

Aidha mama wajawazito wanatakiwa kuwahi kliniki ambako watafuatiliwa maendeleo yao ili kubaini dalili za mwanzo za kifafa cha mimba na kushauriwa kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi.