TEHRAN,IRAN

RAIS wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amekataa pendekezo la Marekani la kutaka kurejeshwa vikwazo vyote vya Umoja huo kwa Iran, uamuzi ambao Washington imesema unalenga kuunga mkono Magaidi.

Balozi wa Indonesia kwenye Umoja wa Mataifa,ambaye nchi yake ndiyo mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama,alisema uamuzi huo ulifikiwa baada ya wajumbe walio wengi kupinga juhudi hiyo ya Marekani dhidi ya Iran.

Mataifa mengine wanachama wa Baraza la Usalama isipokuwa Jamhuri ya Dominica yalisema pendekezo la Marekani ni kinyume na sheria kwa sababu nchi hiyo ilijitoa kwenye mkataba wa nyuklia na Iran mwaka 2018.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo alisema pendekezo la nchi yake lina msingi wa kisheria licha ya Marekani kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya Iran na madola sita yenye nguvu.