LONDON, England

MANCHESTER United, inayonolewa na kocha mkuu, Ole Gunnar bado ina matumaini ya kupata saini ya winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho licha ya dau lake kuwa kubwa.

Imeripotiwa kuwa United kwa sasa inaendelea kufanya mazungumzo na mabosi wa Dortmund inayoshiriki Bundesliga ili wafanikishe dili la nyota huyo mwenye uwezo wa kucheka na nyavu kuibuka ndani ya Ligi Kuu England.

Kwa msimu wa 2019/20, Sancho mwenye miaka 25 ametupia jumla ya mabao 20 ambayo ni sawa na pasi ambazo ametengeneza jambo ambalo limewavutia zaidi United.

Dau la nyota huyo ni pauni milioni 100 jambo linalowafanya mabosi wa United kugoma kuvunja benki ili kumpata mshambuliaji huyo ambaye dili lake ndani ya timu hiyo linaishi mpaka 2022.