WASHINGTON,MAREKANI

MSEMAJI  wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kupigwa risasi kwa Mmarekani Mweusi, katika jimbo la Wisconsin kumezusha maandamano mapya na hivyo lazima kuchunguzwe kwa ukamilifu.

Jumapili iliyopita Jacob Blake, aliyekuwa na umri wa miaka 29, alipigwa risasi na polisi mzungu mjini Kenosha,huko Wisconsin.

Vidio iliyoonekana katika mitandao ya kijamii ilionesha Blake akipigwa risasi mgongoni.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa anasema ubaguzi wa rangi unapaswa kudhibitiwa katika kila jamii, iwe Marekani au kwengineko kokote duniani.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kusema kuwa ni muhimu watu waoneshe hisia zao kwa namna ya amani, kwa vile wana haki hiyo.

Baadhi ya michuano ya michezo kadhaa nchini Marekani ukiwemo wa kikapu ilisitishwa kupinga kitendo cha kupigwa risasi Blake