NA MWAJUMA JUMA

TIMU za soka za Urafiki na Sebleni zimeshindwa kutamba katika michezo yao ya ligi daraja la pili wilaya ya Mjini hatua ya nane bora iliyochezwa juzi.

Timu hizo zilishuka katika viwanja vya Mao Zedong kwa nyakati tofauti ambapo Urafiki ilifungwa na Shangani mabao 2-1.

Mchezo huo uliooneshwa upinzani wa hali ya juu ulichezwa kwenye uwanja wa Mao Zedong B saa 8:00 za mchana.

Kwa upande wa timu ya Sebleni ilishuka katika uwanja wa Mao Zedong saa 10:00 za jioni ilifungwa na Negro United mabao 3-1.

Shangani katika mchezo huo mabao yake yalifungwa na Yussuf Said Ibrahim ambae alifunga katika dakika ya nane na 47 na la Urafiki lilifungwa na Kombo Said dakika ya 43.

Nayo ligi  daraja la tatu wilaya ya Mjini Unguja iliendelea tena juzi kwa kupigwa michezo miwili kwenye kiwanja cha KMKM Maisara.

Michezo hiyo iliwakutanisha Sicco na Ziwatuwe ambao saa 8: 00 mchana na kumalizika kwa Ziwatuwe kufungwa mabao 2-1.

Mchezo mwengine a ulichezwa uwanjani hapo baina ya  Super Eagle na Mwembemakumbi, ambao ulimalizika kwa wanaume hao kutoka sare ya kufungana bao 1-1.