ANKARA,UTURUKI

UTURUKI jana imekosoa makubaliano baina ya vikosi vya kijeshi vinavyoongozwa na Syria pamoja na kampuni moja ya mafuta ya Marekani kama yasiyokubalika na kusema ni sawa na kufadhili ugaidi.

Maofisa wa ngazi ya juu wa Marekani walithibitisha kuwa kampuni hiyo ya Marekani ilisaini makubaliano na wanajeshi wa Syrian Democratic Forces SDF kwa ajili ya kuvitengeneza visima vya mafuta kuwa vya kisasa.

Syria ililaani makubaliano hayo ikisema ni wizi na uingiliwaji wa uhuru wake wa kitaifa.

Wapiganaji wa SDF wanaoungwa mkono na Marekani wanadhibiti visima vikubwa vya mafuta nchini Syria na kundi hilo linajumuisha wanamgambo wa Syria ambao Uturuki inawachukulia kama kundi la kigaidi lililo na muungano na chama cha Kurdistan Workers Party PKK.