NA MADINA ISSA
TAASISIS inayoratibu huduma za kijamii ya nchini Uturuki kwa kushirikiana na taasisi inayoshughulikia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, imetoa nguo kwa ajili ya wauguzi wa hospitali za serikali Unguja na Pemba.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano yaliyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja, Mkurugenzi Idara ya tiba Dk.Juma Salum Mambi, alisema misaada inayotolewa hasa katika sekta ya afya inasaidia kuimarisha huduma bora kwa wananchi.
Aidha alisema pamoja na serikali kuwa na bajeti ya kutekeleza mambo muhimu kwa sekta hiyo, lakini bado kunahitajika nguvu ya pamoja kutoka katika taasisi kama hizo, ili kutoa huduma zitakazokidhi mahitaji ya wananchi kwa wakati.
Alisema kuwa msaada huo utaweza kufikishwa kwa walengwa ili lengo la kutolewa lifikiwe, pamoja na kuwapongeza kwa imani yao kuwapelekea msada huo.
Nae, Afisa muanzilishi wa taasisi inayoshughulikia watoto wanaozaliwa bila ya wakati Doris Mollel, alishukuru serikali kwa kuiamini taasisi hiyo na kupokea msaada mbalimbali wanayoitoa katika taasisi yao.
Kwa upande wake Mratibu wa taasisi ya C tika, Badru Yasir Kassim, alisema taasisi yake imekuwa inafanya kazi za kijamii zaidi kupitia sekta za afya, elimu na kilimo kwa kutambua kuwa ni miongoni mwa maeneo yenye vikwazo na yanayoigusa jamii moja kwa moja.
Hivyo, aliahidi kuendelea kutoa misaada kila inapotumika, ili kuweza kusaidia wananchi katika kuwasaidia wananchi wanaohitaji msaada.
Msaada huo wa nguo kwa ajili ya wahudumu wa hospitali za serikali zipatazo 400 zimeharimu jumla ya shilingi milioni 35.