NA MARYAM SALUM, PEMBA
WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Kusini
Pemba, wamefanya uteuzi wa kuwapata madiwani ambao watakiongoza Chama hicho kwa miaka mitano ijayo.
Katibu mwenezi mkoa huo , Khatib Haji Khalid, amesema kuwa wajumbe wa
halmashauri kuu mkoa Kusini Pemba, imefanikiwa kuwapitisha wagombea wa
nafasi za Udiwani pamoja na UWT kwa mkoa huo.
Alisema kuwa Kamati ya maadili ilikaa pamoja na kupeana mashirikiano
yakutosha ili kuhakikisha wanafanya mchakato huo na kutoa haki kwa
kila mtu bila kufanya upendeleo wowote.
“Kamati imekaa pamoja kuteua wagombea waliogombea nafasi mbali mbali
za uongozi ikiwemo Udiwani pamoja UWT ndani ya Mkoa, kwa kufuata ibara
ya 89 (10) kifungu kidogo cha d , bila ya kumuone mtu, kwani
tumeteua kwa mujibu wa sheria zinavyoelekeza,” alisema mwenezi huyo.
Alifahamisha kuwa wanachama ambao wameteuliwa kugombea nafasi za
Udiwani wa Wadi na Viti maaalum mwaka 2020, kwa Wadi ya Mkoani ni Ali
Abdalla Ngairo, Wadi ya Chokocho ni Rajabu Ali Ussi, Wadi ya
Michenzani ni Mashavu Amour Mohamed, Wadi ya Mtambile ni Mwadini Ali
Mwadini.
Wadi ya Kangani ni Mayasa Said Makame, Wadi ya Kendwa ni Kimanga
Ramadhani Msabah, Wadi ya Kengeja ni Juma Muhamed Juma, na Wadi ya
Ngwachani ni Mohamed Said Ali, Wadi ya Dodo ni Zuwena Hassan
Kaduara.
Kwa upande wa Wilaya ya Chake Chake walioteuliwa , kwa Wadi ya
Vitongoji ni Hamad Abdalla Hamad, Wadi ya Ole ni Khadija Henock
Maziku, wadi ya Wara ni Kassim Juma Khamis, wadi ya Kibokoni ni Ali
Yussuf Juma, wadi ya Ndagoni ni Arafa Kassim Abass, wadi ya kwale ni
Khamis Maneno Mohamed.
Nyengine ni wadi ya Madungu ambaye ni Rashid Khamis Yussuf, Wadi ya
Tibirinzi ni Fatma Juma Khamis, wadi ya Matale ni Time Ramadhani
Khatib, na wadi ya Kilindi ni Juma Hamad Makame.
Kwa upande wa Udiwani viti maaalum (UWT) Wilaya ya Mkoani walioeuliwa
ni Hasina Sharif Mohamed, Fatma Mohamed Bakar, Rahma Ali Mohamed na
Fatma Khamis Othaman.
Wilaya ya Chake Chake viti maalum (UWT) ni Rahima Khamis Haji, Asha
Khamis Omar, Zuhura Juma Maalim, na Adila Juma Suleiman, ambapo jumla
ya wagombea wote walikuwa 115.
Hivyo alitowa wito kwa wanachama wa CCM ambao hawakubahatika kupata
nafasi katika kinyang’anyiro hicho waone kuwa kura hazikutosha na
hivyo waendelee kutowa ushirikiano sambamba na kuvunja makundi ili
Chama kiweze kusonga mbele.