LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Jamie Vardy, amekubali dili jipya ambalo litamuweka klabuni hapo hadi 2023.

Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 hapo ‘King Power’ lilikuwa linamalizika kwenye miaka miwili.

Hata hivyo, Vardy alizawadiwa nyongeza ya mwaka mmoja baada ya kumaliza msimu uliopita akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Englanda akiwa na mabao 23.
“Ni hisia maalum kuwa na uwezo wa kutekeleza maisha yangu ya baadaye kwa Leicester City kwa mara nyengine,” Vardy, alisema.

“Ninapenda kucheza mpira wangu mbele ya mashabiki wetu kwenye uwanja wa King Power na ninafurahi kuendelea na safari hii wakati wa kufurahisha kwa klabu.
“Tuna timu nzuri ambayo naamini ina uwezo mzuri na siwezi kungojea kuona nini tunaweza kufikia pamoja katika miaka michache ijayo”.(Goal).