NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya Ngome FC imetoka kidedea baada ya kuifunga Muembemakumbi mabao 3-1, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kanda ya Unguja uliochezwa juzi uwanja wa Mao Zedong.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani  ulichezwa majira ya saa 10:00 za jioni ambapo Ngome, walitangulia kupata bao la mapema dakika ya 16 kupitia kwa Khalfan Ali Abdalla.

Ngome waliendelea kushambuliana na Muembemakumbi kufanikiwa kusawazisha bao hilo mnamo dakika ya 37 kupitia kwa Salum Juma Saleh.

Hadi wanakwenda mapumziko miamba hiyo ilikuwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kipindi cha pili dakika ya 60 Ngome walipata bao la pili lililofungwa na Is-haka Amour Haji na dakika ya 67 wakafunga bao la tatu kupitia Makame Hamad Mbwana.

Ligi hiyo leo itaendelea tena kwa kupigwa michezo mitatu ambao katika uwanja wa Mao Zedong A saa 8:00 mchana Ngome itashuka tena kuumana na Miembeni, saa 10:00 za alaasiri Uhamiaji itacheza na Dulla Boys Mao Zedong B na saa 8:00 mchana uwanjani hapo Muembemakumbi itakipiga na

Bweleo.