BERLIN,UJERUMANI

IDADI  ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani imepanda na kufikia viwango vya mwanzoni mwa mwezi Mei.

Kwa mujibu wa taasisi ya afya ya Robert Koch RKI, visa vipya 1,226 vya maambukizi viliripotiwa katika muda wa siku moja.

Idadi ya mwisho ya juu iliripotiwa tarehe 9 Mei. Tofauti na hapo kabla, ongezeko la sasa halitokani na maambukizi ya eneo moja moja bali nchi nzima.

Wataalamu wanahofia hatua hiyo kwa sababu haiwezi kudhibitiwa kwa kuchukuliwa hatua chache kali.

Rais wa RKI, Lothar Wieler alitaja uzembe wa kutekeleza agizo la uvaaji wa lazima wa barakoa, kuweka umbali kati ya mtu na mtu na usafi kuwa vyanzo vya ongezeko hilo la maambukizi.