NEW DELHI,INDIA

IDADI ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni imepindukia milioni 20.

Idadi hii ni kulingana na chuo kikuu cha John Hopkins cha nchini Marekani.

Miongoni mwa visa hivyo milioni 20, 001,019 vilivyorikodiwa kote ulimweguni na watafiti, zaidi ya milioni tano vilirikodiwa nchini Marekani, sawa na zaidi ya robo ya maambukizi jumla.

Brazil na India zinafuatia kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya kati ya milioni tatu na milioni 2.2. Hadi sasa zaidi ya watu 733,000 walikuwa wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha maradhi ya COVID-19.