NA AMEIR KHALID
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa amesema serikali imendaa mpango maalum wa kuvifahamu visiwa vidogo vinavyotumika na visivyotumika.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kufahamu jinsi gani serikali inaweza kuvitumia na kuviendeleza visiwa hivyo kwa njia tofauti ikiwemo uwekezaji na shughuli za kijamii kwa ajili kuongeza mapato.


Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea visiwa vya Bawe na Chumbe.
“Zanzibar ina visiwa vingi na haiwezekani vyote kuwa vya uvuvi, lazima baadhi yao viwe vya uwekezaji na vyengine wananchi wavitumie kwa ajili ya shughuli zao za kujitafutia riziki,” alieleza Waziri Abdiwawa.


Akitoa maelezo Mtunzaji Mkuu wa kisiwa cha Chumbe Omar Nyange alisema utunzaji wa kisiwa hicho umeanza mwaka 1992 na mwaka 1994 ikatangazwa rasmi kuwa hifadhi maalumu na mwaka 1998 ilizifuguliwa rasmi na aliyekuwa Waziri wa Utalii, Biasahara na Uwezekezaji Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Tanzania.


Alisema hifadhi hiyo ina zaidi ya Matumbawe 200 na samaki wa aina mbali mbali zaidi ya 400, jambo ambalo linaifanya hifadhi kuwa ya kipekee na kushinda tunzo mbalimbali za dunia ya hifadhi ya kimazingira.


Hata hivyo ameiomba serikali itowe elimu zaidi ya umuhimu wa hifadhi hiyo ambayo kama itatunzwa basi itasaidia pato kubwa la taifa.
Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wagumu kufuata sheria za hifadhi ya kisiwa hicho hasa wavuvi, hivyo ni vyema Serikali ikasaidia kutoa elimu wananchi wafahamu umuhimu wa hifadhi.
Kwa upande wake Meneja wa kisiwa cha utalii cha Bawe Habel Mnjau, ameshukuru kupata ujumbe huo kwani amepata kuzungumzia changamoto zinazowakabili, ambazo ana imani serikali itasaidia kuzitatua.


Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wagumu kufuata sheria za hifadhi ya kisiwa hicho hasa wavuvi, hivyo ni vyema Serikali ikasaidia kutoa elimu wananchi wafahamu umuhimu wa hifadhi.
Kwa upande wake Meneja wa kisiwa cha utalii cha Bawe Habel Mnjau, ameshukuru kupata ujumbe huo kwani amepata kuzungumzia changamoto zinazowakabili, ambazo ana imani serikali itasaidia kuzitatua.


Alizitaja baadhi ya changamoto hizo ni kuwepo uharibifu wa wa bomba ya maji ambayo ipo chini ya bahari, pamoja na wavuvi kupitsha nyavu kwenye sehemu za matumbawe a kuharibu mazingira.


Kwa upande wake Mkurugenzi Uwekezaji, Uwezeshaji na Miradi ya Uwekezaji Sharif Ali Sharif kutoka Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), alisema katika ziara hiyo wamepata kujiridhisha na uwekezaji uliofanywa kwenye visiwa hivyo.
Alisema kupitia uwekezaji huo, wameridhika namna hifadhi ya mazingira inavyofanyika, na mazingira yanavyotunzwa na kuacha uhalisia wa visiwa hivyo.