NA MWAJUMA JUMA
WAAMUZI vijana wanaofundishwa kituo cha kuendeleza vipaji cha (JKU), wameanza kutumiwa katika michezo ya ligi daraja la kwanza Kanda ya Unguja inayoendelea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mkufunzi wa waamuzi wilaya ya Mjini na kituo hicho Ramadhan Ibada Kibo, alisema waamuzi hao watakuwa wakiwatumia siku za Jumamosi na Jumapili, kwani siku za kawaida wanawapa nafasi ya kuhudhuria msomo ya skuli.
“Kwa mujibu wa makubaliano na mapendekezo na kamati ya waamuzi ya Taifa, tutaanza nao kuwatumia katika michezo ya ligi daraja la kwanza kwa siku hizo ambazo nimezitaja”, alisema.
“Kwa hivyo kuna mechi ambazo zitakuwa zinaangukia Jumamosi na Jumapili vijana hawa ndio watafanya kazi, lakini siku nyengine za kawaida kwa sababu wana shughuli nyengine za skuli, watawapa fursa ya kwenda skuli kama kawaida”, alifahamisha Kibo.
Kibo alieleza kuwa tayari program za waamuzi vijana hao tayari zimeanza na zinaendelea kama kawaida, baada ya Serikali kuruhusu kuendelea kwa michezo na skuli ufunguliwa ambazo huzifanya muda wa jioni.
Alisema katika darasa hilo vijana hao wana umri tofauti ambapo baadhi yao, umri wao unawaruhusu kuchezesha madaraja ya watu wazima.
Alisema vijana hao waligawiwa makundi mawili ambapo wapo wana uwezo mkubwa wa kuchezesha madaraja makubwa