BANGKOK,THAILAND

WAANDAMANAJI 10,000 walikusanyika katika mji mkuu wa Thailand Bangkok wakitaka Waziri mkuu Prayuth Chan-ocha kufanya mageuzi.

Maandamano hayo yanayoongozwa na wanafunzi yaliyozuka mwezi mmoja uliopita na yamekuwa yakifanyika kila siku tangu wakati huo.

Hata hivyo kulingana na sheria za nchi hiyo,yoyote anayekosoa utawala wa kifalme anakabiliwa na adhabu ya kati ya mwaka 1.5 hadi miaka 15 jela.

Waandamanaji pia wanamtaka waziri mkuu Chan-ocha aliyeingia madarakani mwaka 2014 kupitia mapinduzi ya kijeshi kujuzulu.

Taifa hilo limekabiliwa na mapinduzi kadha tangu jeshi lilipoondoa utawala kamili wa kifalme mwaka 1932.

Serikali ilifanya uchaguzi mwaka jana lakini uchaguzi huo unadaiwa kugubikwa na udanganyifu na kuchochea hasira ya umma.