NA ABDI SULEIMAN

WAANDISHI wa Habari wa mazingira nchini, wameshauriwa kufahamu kuwa misitu ni kitu muhimu sana katika suala zima la uhifadhi wa wanyamapori na utalii nchini.

Ushauri huo umetolewa na Afisa mwandamizi kutoka taasisi ya kuzuwia na kupambana na Rushwa Tanzania, Ally Katonya, wakati alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa Mazingira nchin kwa njia ya Mtandao.

Mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Marekani(USAID-Protect), chini ya mradi unaolenga kutoa elimu ya kutokomeza ukatili na ujangili kwa wanyamapori nchini.

Katonya alisema kuwa waandishi wa habari zaidi wamejikita katika masuala ya wanyamapori na kusahau misitu, kuwa ndio chanzo kikubwa cha uingizaji wa fedha nchini.

Alisema serikali iliweza kutaifisha mali zenye thamani ya shilingi Bilioni 4.7, zinazotokana na mazazo ya misitu hivyo ni wazi kwamba misitu ni moja ya rasilimali muhimu katika suala zima la uhifadhi wa wanyamapori.

“Hekta 81 za mazao mbali mbali ya Makurunge yalikamtwa na kuwasilishwa serikalini, tizama mazao hayo yalivyoteketea ni wazi kwamba miti iteketea kwa wingi, hata hii utakataji wa miti na upigaji wa mkaa ni tatizo pia”alisema.

Afisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Salimu Hakim Msemo, alisemamakosa ya ujangili ni miongoni mwa makosa, yanapelekea utakatishaji wa fedha na sheria zipo zinatumika pale watuhumiwa wanapotiwa hatiani.

Alisema kuwepo kwa sheria na watuhumiwa kuwatia hatiani na waandishi wa habari kuandika habari hizo, kumepelekea kupungua kwa masuala ya ujangili nchini, ikiwemo kesi ya malkia wa Tembo ambayo iligonga sana katika vyombo vya habari.

Aidha Msemo alizitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni, sheria ya uhifadhi wa wanyamapori, sheria ya misitu, sheria ya uhifadhi wa taifa, sheria mahususi inayohusika na eneo la ngoro ngoro na sheria ya mazingira, sheria ya utakatishaji wa fedha.