MADRID, Hispania

KLABU ya Atletico Madrid, imethibitisha kwamba, wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza wana corona.

Atletico Madrid inajiandaa kuikabili RB Leipzig katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Alhamisi ya wiki hii nchini Ureno.

 Taarifa ya klabu hiyo iliyotoka Jumamosi iliyopita inaeleza kwamba, baada ya kufanyiwa vipimo, ikagundulika kuwa wachezaji wawili wana corona.

“Miongoni mwa majibu yaliyotoka  jana ni kwamba, wachezaji wawili wamegundulika kuwa na virusi vya corona, tumewaweka sehemu maalum, kwa haraka tumewasiliana na mamlaka ya afya ya Hispania na Ureno, UEFA, Chama cha Soka Hispania, Chama cha Soka Ureno na mamlaka za juu za soka,” ilisema taarifa hiyo bila ya kuainisha majina ya wachezaji hao.