BEIRUT,LEBANON

SIKU mbili baada ya mripuko mkubwa eneo la bandari katika mji mkuu wa Lebanon ,Beirut wafanyakazi 16 wa bandari hiyo walioko pwani ya  bahari ya Mediterania wamekamatwa.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa jeshi la nchi hiyo Faki Akiki, alisema uchunguzi unafanyika dhidi ya maofisa wa bandari pamoja na wa forodha.

Serikali ya Lebanon , ambayo inakabiliwa na mbinyo mkubwa kutoka kwa umma wa nchi hiyo,iliahidi kutoa maelezo ya haraka kuhusiana na chanzo cha mripuko huo.

Wengi wa wananchi wa nchi hiyo wanataka ufanyike uchunguzi wa kimataifa.

Wafanyakazi wa uokozi wanajaribu kuwatafuta watu 100 ambao hawajulikani waliko.

Idadi ya watu waliofariki kwa mujibu wa Wizara ya afya imepanda na kufikia watu 149.