VALLETTA, MALTA

VIKOSI vya pwani ya Malta juzi viliwaokoa kundi la wahamiaji 118 wakiwemo  wanawake 10, watoto na watoto watano, baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Malta.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Byron Camilleri, alisema wahamiaji hao walikuwa katika hekaheka ya kujiokoa na ndipo vikosi vya mwambao vilivyokuwa doria kujwaona na kuwaokoa.

“Wengi wao walikuwa katika hatari ya kuzama lakini vikosi vyetu viliwaona na kuwaokoa”, alisema.

Katika ujumbe uliorekodiwa kwenye Facebook, Camilleri alisema askari wa jeshi “walishinikizwa” kutekeleza uokoaji kwani watu hao walikuwa kwenye hatari kubwa ya kuzama.

“Vikosi vyenye Silaha vya Malta vililazimishwa kuleta wahamiaji ambao walikuwa wamezama katika eneo la pwani hiyo ya Malta wakiwemo wanawake kumi, mmoja wao akiwa na mtoto mchanga na watoto watano”, ilisema taarifa hiyo.

Hata hivyo, waziri huyo alisema mara baada ya zoezi la uokoaji wahamiaji hao walilazimika kutengwa na kuwekwa kizuizini kwa ajili ya janga la corona.

Camilleri alisema kuwa katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, viongozi wa Libya walikuwa wamewashiikilia wahamiaji 7,000 waliokuwa wakijaribu kuvuka bahari kuelekea Ulaya.