‎ABIDJAN, Ivory Coast
KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Ivory Coast (FIF), imemuengua mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa FIF kwa sababu ya kudaiwa ‘taarifa’ zake hazikukidhi vigezo.

Drogba inadaiwa ndio anapewa kipaumbele zaidi katika mbio za kuwania urais wa FIF katika uchaguzi mkuu wa FIF unaotarajia kufanyika Septemba 5, 2020.
Kwa kuenguliwa huko, Drogba amepoteza nafasi ya kuwania nafasi hiyo ya urais na kumuacha, Sory Diabate na Idriss Diallo katika nafasi.

Drogba alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa kiongozi katika uchaguzi huo, lakini, wajumbe wamehitimisha safari ya nyota huyo wa zamani wa Chelsea.(Goal).