BEIRUT, LEBANON

UCHUNGUZI wa kisheria kuhusu mripuko uliotokea katika bandari ya Beirut nchini Lebanon umeanza kwa mvutano wa kisiasa kuhusiano na uteuzi wa kiongozi wa uchunguzi huo.

Jeshi kutoa vitisho kuwafunga jela wafichuaji pamoja na shaka juu ya iwapo jopo lililoteuliwa kwa misingi ya kidini linaweza kutoa uamuzi bila kuelemea upande wowote.

Hadi sasa Walebanon wengi,matumaini yao makubwa kwa ajili ya kupata majibu sahihi juu ya mripuko ambao uliharibu eneo la mji wao mkuu huenda yako kwa watu wa nje.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa idadi ya waliofariki kutokana na mripuko huo imefikia watu 180, ambao wanakadiriwa watu 6000 wamejeruhiwa na kiasi ya watu wengine 30 hawajulikani waliko.