KIGALI,RWANDA

WALINDA Amani nchini Rwanda wamepatiwa kituo kipya chini ya ujumbe wa pamoja wa Ujumuishaji wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya kati (MINUSCA) kwa kushirikiana na maofisa wa MINUSCA.

Walinda amani hao walikabidhiwa jengo jipya katika mji wa Bria, Haute Kotto.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda, ilieleza kuwa kituo hicho kina vyumba nne vya kulala, sebule na bafuni kituo hicho kimegharimu dola za kimarekani 40,767.

Ofisa wa uendelezaji wa kikosi cha vita vya Rwanda Lt Col Leodomir Uwizeyimana alisema kuwa mradi huo ulikusudiwa kuboresha uwezo wa kuwakaribisha wageni wa muda wa mkoa huo.

“Ninashukuru sana kwa kituo hiki kwa walinda amani wa Rwanda,ni ishara ya udugu jengo hilo litasaidia kutunza maofisa wakuu ambao watatembelea mkoa wetu,”alisema.

Ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya miradi yenye faida za haraka katika kusaidia jamii na ilianzishwa na kutekelezwa na walinda amani wa Rwanda kwa msaada kamili kutoka kwa MINUSCA.

Rwanda imekuwa ikihifadhi walinda amani huko CAR tangu mwaka 2014 na mbali na jeshi, nchi hiyo inashikilia polisi wakiwa katika jimbo kuu la Afrika.