ZASPOTI
NDIVYO unaweza kusema kwa maneno mafupi.Arsenal mabingwa wapya Kombe la FA.
Mtaalamu nyota wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, amefanyakazi tena ya uchawi wake kwenye uwanja wa Wembley huku wakitoka nyuma na kuichapa Chelsea magoli 2-1 na kushinda Kombe la FA kwa rekodi ya mara 14.

Chelsea iliongoza katika mchezo huo wa fainali ya Kombe la FA ndani ya dakika tano kupitia Christian Pulisic aliyemalizia vizuri, lakini, kisha ikaangushwa na kipaji cha Aubameyang, ambaye pia alikuwa shujaa wa Arsenal wakati alipofunga mara mbili kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Manchester City.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon aliisawazishia Arsenal kwa mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa vibaya na nahodha wa Chelsea, Cesar Azpilicueta, kisha akafunga goli la kiwango cha juu kwenye mechi hiyo iliyochezwa bila ya mashabiki kwa mara ya kwanza.

Chelsea walianza mchezo vizuri kabla ya kulizidiwa baada ya maumivu ya Azpilicueta aliyelazimika kutolewa nje na pia walipompoteza Pulisic baada ya mapumziko.
Huku ‘the Blues’ wakipambana kushinda shida hizo, kipaji cha Aubameyang kilimnufaisha, Mikel Arteta kwa kumpa taji katika msimu wake wa kwanza kama meneja wa washika bunduki hao.

Aubameyang, ambaye Arsenal wanasababu ya kupata salama kwenye mkataba mpya wa muda mrefu, alimzidi ujanja beki wa Chelsea, Kurt Zouma kwenye dakika ya 67 kabla ya kumalizia kazi akimchambua mlinda mlango, Willy Caballero, kutoka pembeni ya lango.
Uchungu wa Chelsea uliongezeka zaidi wakati Mateo Kovacic alipotolewa nje kwa kadi ya pili ya njano, iliyotolewa na mwamuzi, Anthony Taylor, kwa changamoto zisizokubalika dhidi ya Granit Xhaka.

Arsenal tayari imejihakikishia kupata nafasi katika Ligi ya Europa msimu ujao, lakini, ilikuwa uchungu mkubwa kwa meneja wa Chelsea, Frank Lampard wakati wa kuhitimisha kampeni yake ya kwanza akiwa madarakani.

Arteta alifurahia baada ya firimbi ya mwisho na ilikuwa dhahiri akipata taji lake kubwa la kwanza kama meneja baada ya kufanikiwa kurithi mikoba ya Unai Emery mnamo Disemba.
Kumekuwa na wakati wa mchanganyiko, lakini katika wiki za hivi karibuni, Arsenal wameonyesha maendeleo yao kwa kuwashinda mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England, Liverpool na kumaliza matarajio ya Manchester City ya kutetea taji la Kombe la FA kwa kuwachapa na kufikia fainali. Sasa washika bunduki hao wana taji mikononi mwao baada ya kuitolea nje Chelsea.

Katika kila mchezo walionyesha tabia, ujasiri na ushujaa, sifa zote ambazo walishutumiwa mara kwa mara kwa kuzikosa na kuwa na silaha ya kiwango cha ulimwengu, Aubameyang.
Mchezaji ambaye hufanya tofauti katika michezo mikubwa. Aubameyang ameonyesha kuwa, ameufanya Wembley kuwa uwanja wake wa kucheza katika nusu fainali na fainali.
Aubameyang kwa mara nyengine amethibitisha thamani yake kwa Arsenal akiwasaidia kubeba taji lao la kwanza kubwa tokea mwaka 2017 huku Arteta akiandika historia kwenye vitabu vya washika bunduki hao.

Arteta amekuwa mtu wa kwanza akiwa nahodha na kuinoa Arsenal kupata ushindi kwenye fainali ya Kombe la FA wakati Chelsea wamepoteza mechi zao tatu za fainali katika mechi 10 za FA na vipigo vyote vitatu vilikuja dhidi ya Arsenal.
Tangu aanze mechi yake ya kwanza akiwa na Arsenal mnamo Februari 2018, Aubameyang ameshafunga mabao 70 katika mashindano yote, zaidi ya mchezaji mwengine yeyote wa Ligi Kuu ya Engalnd wakati huo.
Aidha, goli la Pulisic lilikuwa la kwanza kwenye fainali ya FA kufungwa na mchezaji wa Marekani huku

Mateo Kovacic, akawa mchezaji wa sita kufurushwa nje ya uwanja katika fainali ya FA na wawili waliopita walikuwa wachezaji wa Chelsea, (Victor Moses, alitolewa dhidi ya Arsenal, 2017).
Wakati huo huo, Arteta, amesema klabu yake inatakiwa kuiga utamaduni wa kushinda ambao wamekuwa nao wapinzani wao Chelsea katika miaka 15 iliyopita.
Chelsea imetwaa mataji 16 tangu Roman Abramovich alipofanya uwekezaji kwenye klabu hiyo 2003 na hakuna timu nyingine ya England ambayo inaweza kulinganishwa nayo tangu wakati huo.

Lakini, meneja wa sasa wa Chelsea, Frank Lampard, ni meneja wa 12 chini ya utawala wa Abramovich.
“Wamenolewa na makocha wazuri. Kabla ya Abramovich, haikuwa timu ya kushinda. Lakini walifanikiwa kubadilisha mawazo na kuwashawishi wachezaji na kuweka shinikizo kwa kila mtu kwenye klabu kwamba lengo pekee kwao ni kushinda”.
“Mambo yakiwa hivyo unakuta kila mmoja anafanya vizuri”.
Arsenal haikuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu ya England, ikimaliza katika nafasi ya nane baada ya kujikusanyia pointi 56.(BBC Sports).