NAIROBI,KENYA
KARIBU watu 48 wa familia moja wamegundulika kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona baada ya mmoja wao kusafiri kutoka Nairobi kwenda kuungana nao .
Katibu wa Baraza la Mawaziri la Afya Mutahi Kagwe alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila siku kuhusu Covid-19.
Kagwe alithibitisha maambukizo hayo alipotangaza kesi mpya 671 za Covid-19,na 633 kati ya kesi hizo mpya walikuwa Wakenya na wageni 33.
Nairobi inaendelea kuongoza na kesi mpya zaidi ya 19 za Covid-19,ikifuatiwa na Kiambu 112, Machakos 20, Kisumu 16 na Mombasa sita.
Wagonjwa wengine 603 walipona virusi vya corona,na kufanya jumla ya wagonjwa waliopona kwa Kenya kuwa 9,930,436 walikuwa kwenye matunzo ya nyumbani na 167 walitolewa Hospitali mbalimbali.
Vifo vya Covid-19 nchini vilifikia 391 baada ya wagonjwa wengine watatu kufa.