MINSK,BELARUS

WAENDESHA  mashitaka nchini Belarus wameanzisha uchunguzi dhidi ya wanaharakati wa upinzani waliounda baraza la kujadili kukabidhi mamlaka kidemokrasia wakati maandamano makubwa ya kupinga matokeo ya uchaguzi yakiwa yanaendelea.

Mwendesha mashitaka mkuu wa Belarus alisema kubuniwa kwa baraza hilo lililokutana kwa mara ya kwanza hapo juzi ni kinyume na katiba.

Wanachama wa baraza hilo walikanusha mashitaka hayo wakisema hatua waliochukua inaenda sambamba na sheria za nchi hiyo.

Matokeo hayo yalimuongezea muda dikteta Alexander Lukashenko aliyeiongoza nchi hiyo kwa miaka 26.

Lukashenko aliwapuuza waandamanaji wanaotaka kujiuzulu kwake akisema wanachochewa na nchi za Magharibi.

Alikuwa amewatishia viongozi wa upinzani kwamba atawafungulia mashtaka ya uhalifu.