JAMMU, KASHMIR

WANAMGAMBO  wameshambulia kikosi cha polisi katika eneo la Kashmir jana, wakiwauwa maofisa wawili na kumjeruhi mmoja licha ya usalama mkali uliowekwa katika jimbo hilo linalogombaniwa.

Eneo hilo wakaazi wake wengi ni Waislamu, kabla ya siku ya uhuru ya India.

Mkuu wa polisi wa Kashmir,Vijay Kumar alisema kundi la wanamgambo limefyatua risasi dhidi ya kundi la polisi ambalo lilikuwa likilinda doria katika eneo la Nowgam la mji wa Srinagar.

Shambulio hilo linatokea siku chache baada ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuondolewa kwa mamlaka ya kikatiba katika jimbo hilo, mageuzi ambayo Serikali ya India inasema yataleta maendeleo katika jimbo hilo kwa kuileta karibu na eneo lote la nchi ya India.