NA MADINA ISSA

WANANCHI wa Zanzibar wameshauriwa kuvitangaza zaidi vivutio vya utalii na maeneo ya kihistoria yaliopo katika visiwa hivyo, ili kuendeleza kukuza utalii uliokuwepo.

Ushauri huo umetolewa na mmoja wa wanachama wa Jumuiya taasisi ya kushajihisha utalii wa ndani ZANRISM, wakati wakiwa katika ziara ya kutembelea maeneo ya utalii na ya historia ya Zanzibar.

Alisema endapo wananchi watakapojitokeza wataweza kuendeleza kuutangaza utalii wa ndani ambao ni tegemeo la nchi na kuendeleza pato la Taifa.

Aidha alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali ili kuona utalii unakuwa nchini pamoja na kuyafanyia marekebisho baadhi ya majengo ili kuweza kuimarisha zaidi.

Hata hivyo, alisema kuwa ni vyema Juhudi mbali mbali zikachukuliwa ili kuendelea kukuza sekta ya utalii nchini ambapo kwa sasa pato limeengezeka kwa asilimia 27 na asilimia 80 ya fedha za kigeni.

Hata hvyo alifahamisha kuwa juhuhudi hizo ni pamoja na Serikali kuruhusu uingiaji wa wageni kutoka nchi mbali mbali baada ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19, sambamba na kuweka sera ya utalii kwa wote ambayo inatoa fursa kwa wenyeji kutembelea maeneo mbali mbali ya utalii.