NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

WANASIASA na wadau wengine wa uchaguzi wanapaswa kuendesha shughuli nzima za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, katika hali ya amani na utulivu bila ya kuingilia majukumu ya nafasi nyengine.

Ni jambo la kawaida kwa nchi ya Tanzania kila baada ya miaka mitano hufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kuwachagua viongozi wa ngazi tofauti wakiwemo wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mgombea wa Urais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani kwa nchi mzima.

Tanzania ilianza kupiga kura kupitia mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 na kuachana na ule mfumo uliozoeleka kwa chama kimoja, ambao ulifutwa mwaka 1992 baada ya kupigwa kura ya maoni na watanzania walioridhia kuwepo kwa vyama vingi vya siasa.

Hivi karibuni mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro aliwaeleza wadau wa vyama vya siasa na tume ya uchaguzi kuwa nchi ipo salama, ambapo takwimu za kiujumla zinaonyesha kumedumishwa hali ya amani na ulituvu nchini.

Jeshi la Polisi lipo tayari kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu unafanyika kwa utulivu na amani.

Uzoefu unaonesha kwamba wakati wa kipindi cha uchaguzi hujitokea baadhi ya changamoto ambazo kwa njia moja ama nyengine zinaathiri usalama katika baadhi ya maeneo hapa nchini.

Hali hiyo inatokana na baadhi ya viongozi wa siasa kushindwa kunadi sera na hujifanya ni wanaharakati kwa kusema maneno ya chuki, udhalilishaji, kejeli, uongo, na vitisho kwa jamii, ni kinyume cha kisheria na utaratibu.

Matumizi mabaya ya habari na teknolojia kwa kufanya makosa ya kiuhalifu ya mtandao, hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa makini katika harakati za siasa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka.

Wakati wa kampeni zinatarajiwa kuanza hivi karibuni ni vyema kwa vyama vya siasa kuzingatia muda wa kuanza kwa kampeni na kumaliza mikutano yao kwa lengo hilo hilo la kudumisha amani.

Hata hivyo tabia ya baadhi ya viongozi wa siasa wanapomaliza mikutano yao ya kampeni huwaamuru wafuasi wao waondoke kwa kuandamana, jambo ambalo sio sahihi kiusalama na wakati mwengine huwapa mwanya wahalifu.

Wapo baadhi ya viongozi wa siasa, ambao husababisha vurugu zisizo na tija kwa kusema wanalinda kura wakati wa uchaguzi, jambo ambalo kisheria haijatamka popote sio katika kanuni wala sheria kuwa walinde kura, ‘unalinda kura kwa sheria ipi’, hivyo Jeshi la Polisi haliwezi kumuacha kwa vile tayari amevunja sheria.

Baadhi ya viongozi wa wanasiasa kuingia katika uchaguzi wa zana hasi ya matokeo na kusababisha mazingira ya uvunjifu wa amani kabla ya matokeo ya uchaguzi.