MINSK,BELARUS

UPINZANI nchini Belarus unapanga kushinikiza kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa,baada ya Rais aliyechaguliwa tena Alexander Lukashenko kulaani maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

Upinzani unapanga kufungua mashitaka juu ya mauaji ya waandamanaji wawili na matumizi ya kupita kiasi ya vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji na wafungwa.

Mpaka sasa watu wapatao 4,000 bado wanashikiliwa kufuatia maandamano yaliyoanza wiki iliyopita ya kupinga matokeo ya uchaguzi.

Rais Lukashenko alisisitiza mbele ya wafuasi wake kuwa hana nia ya kuachia ngazi.

Pia aliituhumu Jumuiya ya kujihami NATO kwa kujiimarisha kijeshi katika eneo la mpaka wa magharibi,lakini jumuiya hiyo ilisema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea nchini humo na kwamba uwepo wa majeshi upande wa Ulaya mashariki siyo kitisho kwa nchi yoyote na unalenga kulinda amani na kuzuia hali ya mizozo.