MINSK,BELARUS

POLISI nchini Belarus imewakamata viongozi kadhaa wa upinzani na waandamanaji walioshiriki wimbi la maandamano yanayopinga matokeo ya uchaguzi yalayompa ushindi Rais Alexander Luakashenko.

Baraza la Uratibu lililoundwa na upande wa upinzani limesema polisi mjini Minsk imewakamata wajumbe wake wawili pamoja na kiongozi wa mgomo uliofanywa na wafanyakazi wa viwandani nchini humo.

Polisi pia inawashikilia karibu watu watano ambao ni miongoni mwa waandamamanaji waliokusanyika kwenye uwanja wa uhuru mjini Minsk huku wengine watano walikamatwa katika miji mengine.

Waendesha mashitaka walisema wote waliokamatwa watashitakiwa kwa kutishia usalama wa taifa, madai ambayo  yalipingwa vikali.

Hatua hizo ni ishara kuwa Serikali ya Rais Lukashenko inalenga kufanya ukandamizaji dhidi ya maandamanao hayo yaliyoingia wiki ya tatu sasa.