GITEGA,BURUNDI

MAHAKAMA ya Burundi imewafunga jela wanaume wawili na mwanamke mmoja kifunfo cha miaka 30 baada ya kumshambulia kwa kurembea mawe kwenye msafara wa Rais Evariste Ndayishimiye.

Upande wa mashitaka,uliiambia Mahakama kuwa mawe matatu yalitupwa kutoka kituo cha petroli kwenye msafara wa magari 50 wakati yakipitia mji wa kaskazini mwa Kayanza wiki iliyopita iliyopita.

Jiwe moja liligonga mmoja wa walinzi wa Rais,jengine likagonga pembeni ya gari na jengine halikugonga chochote.

Mashahidi huko Kayanza waliiambia AFP kuwa msafara huo haukusitaa wakati wa tukio hilo.

Mahakama ya Kayanza iliwahukumu vijana hao watatu akiwemo mwanamke jela miaka 30 gerezani (kila mmoja) kwa shambulio na njama dhidi ya mkuu wa nchi.