KAMPALA,UGANDA

WANASAYANSI  wamethibitisha kutokea kwa vifo vya Covid-19 nchini Uganda na kuongeza kwa maambukizi ndani ya jamii.

Uganda ilikuwa imesajili kesi 1,297 na waliopona 1,137 pamoja na vifo tisa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Ufundi ya Chuo Kikuu cha Makerere,Dk Bruce Kirenga,alisema kwamba kiwango cha kugundua  virusi hivyo kiko juu zaidi katika kesi za jamii, ambaopo  chanzo chake na walipoambukizwa haijulikani.

Alisema hapo awali, kesi hizo zilikuwa zinagunduliwa na kutibiwa mapema lakini tangu kufunguliwa kwa baadhi ya vizuizi, maambukizi ya jamii ni vigumu kugundulika mapema na kutibiwa kwa wakati.

“Tuna kesi za jamii, hatujui ni lini waliambukizwa,hatujui chanzo, kwa hivyo nguvu ya kufunguliwa ni kubwa sana na watu wanapougua hawaendi Hospitali haraka,” Dk.Kirenga alisema.

Dk Kirenga alisema awali,nchi ilikuwa ikipambana na kesi nyingi zinazotokana na madereva wa lori .

“Hapo awali, tuliwapata watu waliokuwa wakiendesha gari kutoka Mombasa”,alisema.

Dk Henry Kajumbula,mshauri wa timu ya kuzuia na kudhibiti maambukizi,alisema vifo hivyo vinaweza kuwa kiashiria cha maambukizo ya jamii yanayoongezeka ambayo yanafichua walio katika hatari ya ugonjwa huo.

“Ikiwa ni katika jamii, basi unapata watu wengi ambao wako hatarini  kama wazee, watu wenye tabia nyengine.Hiyo inaweza kuwa sababu ya maambukizi,”Dk Kajumbula alisema.