NA MWANAJUMA MMANGA

IDARA ya Misitu Maliasili Zisizorejesheka imefanikiwa kuwakamata  watu 10 ambao wanawinda Paa katika msitu wa hifadhi ya Pongwe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema watuhumiwa hao walikuwa wanasafirisha paa watatu kwa kutumia gari aina ya Keri baada ya kumaliza shughuli ya uwindaji wa wanyama hao.

Akizungumza na gazeti hili Msimamizi wa Sheria Maliasili, Madini na Misitu, Haji Haji Hassan, alieleza hayo wakati alipokua akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Maruhubi

Alisema gari hiyo waliyoikamata yenye namba za usajili Z.435 GN aina ya Keri ambayo iliyokuwa imepakia Paa hao na kusafirisha.

Alisema watu hao walikamatwa kufuatia doria iliyofanywa na kikosi cha doria cha Idara hiyo, baada ya kuwepo watu wanaofanya uharibifu wa misitu, uwindaji wa wanyama pamoja na uharibifu wa maliasili zisizorejesheka.

Alisema tukio hilo limetokea Julai 27, mwaka huu, majira ya saa 10 za jioni huko Pongwe, katika msitu wa hifadhi wakiwa wanaendesha msako wa Paa hao.

Alisema kesi dhidi ya watuhumiwa hao wametakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 2, 500,000 na hadi sasa bado hawajalipa ili iwe fundisho kwa watu wengine.