KABUL, AFGHANISTA

KARIBU watu 122 wamefariki na wengine 147 wamejeruhiwa huku wengine kadhaa wakiwa hawajulikani walipo kufuatia mafuriko makubwa katika majimbo 12 ya mashariki ya Afghanistan, ofisi ya waziri wa serikali ya usimamizi wa janga na maswala ya kibinadamu iliripoti.

“Habari ya awali ilionyesha watu 122 wamefariki na 147 wamejeruhiwa na mafuriko tangu Jumanne usiku katika mkoa wa mashariki mwa Afghanistan,” wizara hiyo ilisema katika taarifa yake ya jana.

Ajali za hivi karibuni zilitokea mashariki mwa Kapisa katika jimbo la Panjshir majira ya usiku wakati watu 10 walifariki huko Panjshir, kulingana na vyanzo vya ndani.

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa watu wapatao 85 walifariki na wengine 110 kujeruhiwa siku ya Jumanne usiku katika jimbo lililoathiriwa zaidi la Parwan, ambapo nusu ya mji mkuu wa mkoa wa Charikar uliathiriwa na mafuriko.

“Operesheni ya uokoaji ilimalizika Jumatano usiku katikati mwa Parwan, na operesheni ya uokoaji ilianza siku ya Alkhamis na kwamba waatjhiriwa wengi bado wamepotea,” Ahmad Tameem Azimi, afisa wa usimamizi wa maafa alisema.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa miongoni mwa majeruhi 24 walipoteza maisha wakati wakipatiwa matibabu hospitalini na wengine 37 waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali za Kabul, Wardak, Nangarhar, Logar, Paktia, Paktika, Nuristan, Laghman na Khost.


Wakuu wa maafa na jeshi la Afghanistan wamekuwa wakitoa chakula kilichopikwa na kisicho cha kupikwa na vitu vingine vya misaada kwa familia zilizoathirika tangu mapema Jumatano.

Mafuriko hayo mabaya pia yakaharibu nyumba 1,500, maduka 23, na zaidi ya hekta 1,100 za ardhi ya kilimo katika mkoa huo huku wanyama 600 wa kufugwa walipotea wakati wa mafuriko hayo.

Mara kadhaa Mikoa ya Afghanistan mashariki sio salama kutokana na kukabiliwa na mvua kubwa za misimu jambo ambalo husababisha mafuriko ambayo huharibu miundombinu na ardhi ya kilimo.