MWASHUNGI TAHIR, MAELEZO
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo, ameitaka jamii kupatiwa elimu na kuwekewa utaratibu wa usafi mazingira wanayoishi ili kuepukana na mambo mbalimbali ikiwemo maradhi.


Waziri Kombo alitoa wito huo Mbweni wakati alipozungumza na vikundi vya usafishaji vya WAJAMAMA ambayo ni taasisi ya inayoweka wanawake na watoto katika hali ya usafi na
Alisema jamii inaonaswala la kuimarisha usafi ni la Manispaa pekee dhana inayopaswa kuondoshwa kwani kila binaadamu anahitaji kuishi katika mazingira yaliyo safi hivyo lazima jitihada za kutoa elimu ziendelezwe.


Hata hivyo, alisema iwapo usafi utaimarika katika maeneo mengi nchini, maradhi ya mripuko hayataweza kutokea na kupunguza bajeti ya dawa hali itakayochochea kuongezeka kwa uchumi wa nchi na pato la mtu mmoja mmoja.


“Iwapo usafi utadumishwa, tutakuwa na jamii yenye afya njema ambayo itaepukana na maradhi ya mripuko na hiyo ndio azma ya serikali ya mapinduzi Zanzibar,” alisema Waziri huyo.
Alisema mji unapokuwa safi, mazingira yanapendeza na kuwavutia watalii jambo litakaloongezeka pato la serikali na ajira kwa vijana.


“Changamoto kubwa ni kwamba jamii yatu haina uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa uhifadhi wa takataka ndani ya sehemu maalum inayowekwa na manispaa na hili ndilo linalosababisha kuzagaa kwa taka mjini,” akueleza Kombo.


Nae Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dk. Abdullah Mohamed Juma, alisema Zanzibar inategemea utalii kwani ndio uti wa mgongo hivyo kuna ulazima wa kusafisha mji na kuweka mazingira katika hali ya usafi.


Pia amesema taka ni rasilimali ambayo inasarifiwa duniani na kwa hapa Zanzibar imeanza kukusanya chupa ambazo zishatumika kwa kusarifiwa na nchi za wenzetu taka hufanyiwa baadhi ya mambo mengine kama vile mbolea na umeme.


Mkurugenzi wa Manispaa ya wilaya ya Magharibi ‘B’ Abdullah Said Natepe, aliitaka jamii iache tabia ya kutupa taka ovyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuchafua mazingira.


Zoezi hilo la kusafisha mji ni endelevu lilianza Forodhani, Nungwi, Jambiani na Mbweni na litaendelea kila sehemu katika mji wa Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi ya Safisha Zanzibar na baadhi ya vikundi vya usafi katika manispaa za jiji la Zanzibar.