TOKYO,JAPAN

WAZIRI  mkuu wa Japan Shinzo Abe ametangaza kwamba amejiuzulu kutokana na sababu za kiafya.

Alisema kwamba hataki maradhi alionayo kuingilia kazi yake, na kuomba msamaha kwa raia wa Japan kwa kushindwa kukamilisha muda wake.

Aliugua kwa miaka mingi kutokana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini hali yake imekuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni.

Mwaka uliopita,alikuwa Waziri mkuu wa Japan aliyehudumu kwa kipindi kirefu nchini Japan.Kipindi chake cha kuhudumu kilianza mwaka 2012.

Mwaka 2007,alijiuzulu ghafla alipokuwa Waziri mkuu kutokana na mapambano yake ya ugonjwa huo wa tumbo, ugonjwa hatari ambao ameishi nao tangu alipokuwa kijana.