LONDON,UINGEREZA

SHIRIKA  la Afya Ulimwenguni WHO limesema watoto kuanzia miaka 12 na zaidi wanapaswa kuvaa barakoa kama watu wazima ili kusaidia kukabiliana na janga la COVID-19.

WHO ilisema watoto wenye umri huo wa miaka 12 na zaidi watalazimika kuvaa barakoa wakati ambapo haitakuwa rahisi kuweka umbali wa mita moja kutoka kwa watu wengine hasa katika maeneo yanayokabiliwa na maambukizi makubwa ya virusi vya corona.

Wakati huo huo WHO ilisema watoto kati ya sita na 11 watapaswa kuvaa barakoa kwenye maeneo ambayo ni hatarishi kwa maana kuwa mahala penye misongamano ya watu.

Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto UNICEF na lile la Afya ulimwenguni WHO yalitoa mwongozo huo katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO mnamo tarehe 21 Agosti.