NA ARAFA MOHAMED
JAMII nchini imetakiwa kutozarau dawa zinazotolewa na wataalamu wa Afya, kwa lengo la kujikinga na maradhi mbalimbali yakiwemo matende, minyoo pamoja na kichocho.
Aliyasema hayo Mtowaji elimu ya Afya, Khadija Hussein Uledi, alipokuwa akizungumza na mwadishi wa habari hizi Ofisini kwake Mpendae Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Alisema,kunabaadhi ya watu wamekuwa wakiwakataza watoto wao kutotumia dawa hizo na wao wenyewe kutotumia dawa hizo ,kwa imani ya kuwa utumiaji dawa hizo unasababisha matatizo jambo ambalo sio sahihi.
Aidha alisema kuwa tabia hiyo sio nzuri, na aliwataka waachane na tabia hiyo, kwani dawa hizo zimethibitishwa, na wataalamu wa Afya na hazina tatizo zipo salama kwa matumizi ya binaadamu.
“Sio tabia nzuri kabisa kuwakataza watoto wasitumie dawa hizo kwani dawa hizo hazina tatizo lolote na zimethibitishwa na wataalamu wa afya, na zimetolewa kwa ajili ya kulinda afya za jamii ili ziondokane na maradhi mbalimbali”alisema.
Alifahamisha kuwa dawa hizo zinazotolewa kwa ajili ya kujikinga na maradhi mbalimbali yakiwemo minyoo, kichocho na matende, ili kujenda jamii yenye afya bora na iweze kuondokana na matatizo .