Jeshi la polisi lina wajibu wa kusimamia makosa, kuwatia hatiani wahusika

NA TATU MAKAME

TANZANIA kama zilivyo nchi nyingi dunia iko katika mfumo wa vyama vingi na kwamba takriban tano zilizoshirikisha vyama vingi zimeshafanyika.

Vyama vingi hapa nchini vilianza mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa mwanzo wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995

Lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo wa vyama vingi ni kupanua wigo wa demokrasia na kujenga mazingira demokrasia na utawala bora.

Pamoja na nia nzuri hiyo ya kuanzishwa kwa mfumo huo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa huutumia vibaya jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo makubwa hapa nchini.

Mara nyingi wakati wa chaguzi kuu huripotiwa vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyochangia kuleta vurugu za kisiasa ikiwemo kutumia lugha za matusi na kashfa kwa wafuasi wa vyama vya siasa pamoja na viongozi wao.

Hivyo katika uchaguzi huu ambapo kampeni zinatarajiwa kuanza baadae mwezi huu kufanyika kwa amani na utulivu huku tukijua kuwa kama kuna maisha badala ya uchaguzi.

Kwa kuwa kampeni za uchaguzi zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu, makala haya imetayarisha mambo muhimu ya wananchi/ wapigakura kuyatekeleza kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa 2020.

Makala haya ilifanya mahojiano na kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Haji Abdalla Haji.

MAJUKUMU YA JESHI LA POLISI NCHINI

Jeshi la Polisi ni chombo cha muungano kwa mujibu wa Ibara ya 4 (3) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Polisi limeundwa chini ya sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi sura ya 322 ambayo imebainisha kazi na majukumu ya Jeshi la Polisi kwenye kifungu namba 5 cha sheria hiyo kuwa.

Hata hivyo alisema jukumu la kulinda usalama ndani ya Tanzania,kusimamia sheria na kanuni na kufanya upelelezi wa mokosa ya jinai,kuzuia makosa na kulinda maisha ya watu na mali zao.

WAJIBU WA JESHI LA POLISI KWA VYAMA VYA SIASA KATIKA MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI

Kamanda Haji alisema jeshi la polisi lina jukumu la kuwalinda viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa kama raia wengine hapa nchini bila kujali itikadi zao.

Aidha alisema katika kipindi hicho hairuhusiwi kwa askari polisi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wala kujihusisha na mambo ya siasa isipokuwa kupiga kura tu.

Hata hivyo alisema kusimamia na kudhibiti mikusanyiko yoyote ya watu kwa mujibu wa sheria za polisi ni jambo la kuzingatiwa na jeshi hilo.

“Ili kuhakikisha mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa inafanyika, kumalizika salama na kuhakikisha zoezi la upigaji kura linaenda sawa bila vikwazo au bugudha ni lazima kujipanga kuelekea huko”, alisema.

Aliyataja majukumu mengine kwa jeshi hilo, ni kuhakikisha kuwa vifaa vya kupigia kura vinakuwa salama yaani haviibiwi kughushiwa wala kutekwa katika kipindi hicho cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Sambamba na hilo kamanda huyo alisema jeshi litahakikisha mchakato wa kupiga kura kuhesabiwa na kutangaza matokeo unakuwa huru na haki  huku usalama ukitawala katika mchakato mzima wa kabla na baada ya kupiga kura.

HAKI NA WAJIBU WA MPIGAKURA

Akizungumzia kuhusu kupiga kura, alisema ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania aliyetimiza umri unaokubalika kisheria.

“Kwa mantiki hiyo inaendana na wajibu mbalimbali kwa mpiga kura ikiwemo wajibu wa kujielimisha kuhusu sheria na taratibu zinazohusu mchakato mzima wa uchaguzi pamoja na wajibu wa kutii sheria na taratibu za uchaguzi.