NA NASRA MANZI

LIGI ya mashindano ya Yamle Yamle Cup yanazidi kuchanja mbuga kwa kuzikutanisha timu ya Taifa Tangini dhidi ya Tilalila FC, uliopigwa  majira ya saa 10:00 jioni kwenye dimba la Magirisi.

Pambano lilokuwa na hamasa huku wakiburudishwa na burudani ya Mdundiko kutoka kwa mashabiki wao.

Katika mtanange huo timu ya Taifa Tangini ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwa kuifunga Tilaliala mabao 2-0.

Mabao ya ushindi yaliwekwa wavuni na Abdalla Janga dakika ya 54,wakati bao la mwisho limefungwa na  Mohamed Abdalla mnamo dakika ya 88. Tilalila walijitahidi kusaka bao la kufutia machozi lakini walishindwa, na kujikuta wanatoka uwanjani bila ya majibu.