NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KLABU za Simba na Yanga zinawania saini ya kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambaye amewekwa sokoni na timu yake.

Hivi karibuni Azam FC walitangaza kumeweka sokoni Sure Boy ambaye ameomba kwenda kutafuta changamoto nyingine ya soka kwenye timu tofauti.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji wa kongwe kwenye kikosi hicho cha wanarambaramba.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka Azam kimeeleza kuwa Yanga na Simba wanamtaka mchezaji huyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Yanga ndio ambao wameonyesha nia ya kumchukua muda mrefu, lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti kwani Simba wanataka kuingilia kati usajili huo  kwa gharama yoyote.