NA ASIA MWALIM

MAMLAKA ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar,(ZAECA) imesema itaendelea kutoa elimu kwa jamii, ili kuhakikisha matukio nayohusisha vitendo vya rushwa yanapungua nchini.

Ofisa Elimu kwa Umma, Harrieth Limo, alisema hayo wakati akizungumza na muandishi wa habari hizi huko maonesho ya tatu ya wakulima ya nane nane katika viwanja vya Dole Kizimbani Unguja. 

Alisema mamlaka hiyo inahusika na kupambana na vitendo hivyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi wake chini ya kifungu cha sheria namba 1ya mwaka 2012, ili kuzuia wanao endelea kuhusika na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi wa Zanzibar. 

Aliwasihi wananchi kuwa na muamko wa kujitokeza kutembelea maonesho yanayofanyika nchini, ili kupata elimu inayohusiana na rushwa, kwani ofisi hiyo imejipanga na inatarajia kuondosha vitendo hivyo nchini.

Alisema wapo baadhi ya watendaji wanakwenda kinyume na sheria za kazi, hivyo ni vyema wananchi kuwafichua bila kujali cheo kwani kufanya hivyo itaisaidia kuwa na watumishi bora.

Ofisa huyo alisema mamlaka hiyo imejipanga kunatoa elimu hiyo kwa wananchi wa ngazi tofauti,ofisi  ikwemo maeneo ya kazi ya sekta na taasisi mbalimbali za Serekali na sekta binafsi, ili kupunguza mianya ya rushwa.