LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace WIlfried Zaha ameipuuza video inayosambaa katika mitandao,ambayo inaonyesha winga huyo akisaini Arsenal.

Mchezaji huyo hivi  sasa yupo likizo baada ya msimu wa Ligi Kuu England kumalizika, Anthony Bill, ametupia taarifa kwenye mtandao wa Instagram yake.

Palace wapo tayari kusikiliza ofa ya Zaha msimu huu wa joto lakini wana uwezekano wa kupata zaidi ya pauni milioni 80.

Na Zaha amejitahidi kujiweka pembeni kabisa na video hizo, kwa kudai kuwa hawezi kudhibiti ambacho  watu wengine wanaandika kwenye chaneli zao za mitandao ya kijamii.

‘Ninafurahiya wakati wangu wa kupumzika na siwezi kudhibiti kila kitu ambacho kila mtu hufanya,’ alisema Zaha.