NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
ALIYEWAHI kuwa kocha mkuu wa timu ya Yanga SC ya Ligi Kuu Tanzania Bara , Mwinyi Zahera, amesema amejiunga na klabu ya Gwambina FC, kama meneja wa timu hiyo.
Gwambina yenye makao yake makuu mkoani Mwanza Misungwi, msimu huu wamepanda kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara ya msimu wa 2020/21.
Akizungumza na Zanzibar Leo jana, Zahera alisema watu wengi wanadhani amesajiliwa kama kocha kwenye kikosi hicho na sio kweli bali ni meneja wa timu.
Alisema amesajiliwa kama meneja mkuu wa Gwambina kwaajili ya kuisimamia timu na wachezaji kwenye mambo mbali mbali, ambayo kwa nafasi yake yanamuhusu na amesaini mkataba wa miaka mitatu.
“Nimesajiliwa na Gwambina hivi karibuni na nimefurahi kuwa hapo watu wengi wanadhani mimi nimesajiliwa kama kocha hapana mimi nimeneja mkuu waklabu,” alisema Mwinyi Zahera.