NA ZAINAB ATUPAE

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema itahakikisha inafikisha elimu ya upigaji kura, katika viwanja mbali mbali vya michezo ikiwemo vinavyotumika kwa ligi na mashindano ndondo cup.

Akizungumza na wa waandishi wa habari huko Magirisi ofisa Uchaguzi wilaya Magharibi B Unguja ambae alikuwa mgeni rasmi wa Mashindano ya Yamle Yamle ndondo Cup  Mbaraka Said Hassoun,alisema elimu hiyo itafikishwa kwa vijana wa kiume na wakie.

Alisema mbali na kutoa elimu sehemu mbali mbali Tume imeona kupita katika viwanja vya michezo kuelimisha vijana watakao kuwepo viwanjani hapo.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwataka vijana kufahamu lengo kuu la Uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

“Tuanaimani kubwa ya kufika malengo kwani vijana wengi tumewapa elimu hiyo”alisema.

Alisema Tume ya Uchaguzi imekuwa miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo kwa lengo la kuwahamasisha vijana wote ambao wanafika uwanjani hapo.

“Tumekuwa miongoni mwa wadhamini wa mashindano haya kwani tunaamini vijana wengi wataweza kufaidika na elimu yetu”alisema.

Hivyo aliwataka vijana kuwa kitu kimoja katika kuleta Amani ya nchi yao kwenye uchaguzi mkuu.