JAALA HAJI
TUME ya Uchaguzi ya Zanziba, (ZEC) imewataka wasimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya kuwa makini na kuvipitia vipengele vya Sheria ya Uchaguzi no 4 ya mwaka 2018 na kanuni za uchaguzi za mwaka 2020 ambazo zitawapatia maelekezo mazuri ya kutekeleza majukumu yao katika kusimamia uchaguzi mkuu 2020
Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC Mabruk Jabu Makame, akizugumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wa Wilaya 11 za Zanzibar, alisema shughuli za Uchaguzi Mkuu zinahitaji kuendeshwa kwa kufuata misingi ya Katiba, Sheria na Kanuni za Uchaguzi ili kila mwenye haki aweze kuipata fursa hiyo.
“Waelekezeni vizuri juu ya utaratibu wa kisheria wateuliwa hao bila ya kujali ni nani amefika katika Ofisi yako kupata huduma” alisema
Alifafanua kuwa, mbali ya kuwepo kwa mafanikio makubwa katika kuendesha kazi za Uchaguzi katika hatua mbali mbali, ikiwemo kazi ya Mapitio ya Majimbo ya Uchaguzi ambapo kwa sasa ni 50 badala ya 54.
Alisema uandikishaji wa wapiga kura wapya na uhakiki wa taarifa za wapiga kura , utoaji wa vitambulisho vya Kupigia Kura, lakini pia wanapaswa kuwa makini na waangalifu zaidi katika kazi ya utoaji wa fomu za uteuzi wa Wagombea
Hata hivyo, aliwasisitiza wasimamizi hao kuhakikisha wanafatilia kwa ukaribu kazi ya upigaji kura , kuhesabu na kujumlisha kura katika vituo na majimbo wanayo yasimamia.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Thabit Idarous Faina, alisema madhumuni ya Tume katika kuwapatia mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao katika Uchaguzi Mkuu 2020.
Akiwasilisha mada kuhusu kampeni za Wagombea Mkuu wa Kurugenzi ya Rasilimali Watu, Mipango na Uendeshaji wa ZEC, Saadun Ahmed Khamis, alisisitiza kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi ahakikishe Mikutano yote ya kampeni za Uchaguzi katika Wilaya yake inaendeshwa katika muda na maeneo yaliyoainishwa kisheria.
Mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimazi wa Uchaguzi wa Wilaya yanaendelea kufanyika ikiwa hatua ya utekelezaji wa mpango kazi wa uchaguzi wa kuwapatia mafunzo watendaji wote watakao husika na kazi ya usimamizi wa Uchaguzi