WASHINGTON,MAREKANI

RAIS  wa Marekani Donald Trump kwa mara nyengine amekanusha mchango wa mabadiliko ya tabia nchi katika ongezeko la mioto ya msituni inayoteketeza misitu magharibi mwa nchi yake.

Alisema bila kunukuu ushahidi wowote wa kisayansi kuwa viwango vya joto duniani vitaanza kushuka.

Trump alisema tatizo kuhusiana na mioto hiyo sio mabadiliko ya tabianchi, bali ni utunzaji mbaya wa misitu.

Gavana wa jimbo la California Gavin Newsom aliyempokea Trump jimboni mwake, alikiri kuwepo matatizo katika utunzaji wa misitu, na kusisitiza kuwa tatizo ni kubwa zaidi ya hapo.

Maeneo makubwa ya misitu katika majimbo ya California, Oregon na Washington yaliangamizwa na moto huo ambao pia uliwauwa watu wasiopungua 35.

Mpinzani wa Trump katika uchaguzi ujao, Joe Biden wa chama cha Democratic alimshutumu rais huyo kuwa mchocheaji wa mioto hiyo.